Makazi Insights

JINSI YA KUPUNGUZA MAZALIA YA MENDE NYUMBANI AU HOTELINI

Zingatia andiko hili kama unapitia changamoto ya Mende

Published: 24 November 2025

Makazi Technical Team

JINSI YA KUPUNGUZA MAZALIA YA MENDE NYUMBANI AU HOTELINI

Ili kudhibiti na kupunguza uwepo wa mende katika makazi au maeneo ya biashara, zingatia mambo yafuatayo:


Kudhibiti Maji Machafu


Hakikisha hakuna maji machafu yanayotuama kwenye mifereji ya maji taka, kwenye sinki au kwenye maeneo ya kuoshea vyombo.


Fanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha mifereji haizibiwi.


Kutupa Mabaki ya Vyakula Kwa Usahihi


Hakikisha mabaki ya vyakula yanamwagwa kwenye dustbin maalumu la kuhifadhia taka zinazooza.


Usiachie mabaki ya chakula jikoni, hasa kwenye maeneo ya chini ya meza, pembezoni, au maeneo yaliyofichika.


Kuepuka Kulala na Vyombo Vichafu


Usilaze vyombo vichafu ndani ya nyumba au jikoni.


Osha vyombo mara baada ya matumizi ili kuzuia harufu na mabaki ya chakula yanayovutia mende.


Kuondoa Vifaa Visivyohitajika


Ondoa maboksi, vyombo vilivyovunjika, karatasi, na vitu vingine visivyotumika.


Vitu hivi huunda maficho mazuri kwa mende na wadudu wengine.


Kusafisha Kwa Uangalifu Maeneo Yote ya Jikoni na Makazi


Safisha chini ya friji, jiko, meza, na makabati ambalo mara nyingi huwa maficho ya mende.


Hakikisha usafi wa mara kwa mara hasa nyakati za usiku ambapo wadudu hutoka kwa wingi.


Kwa ushauri zaidi au huduma za kitaalamu za kudhibiti wadudu, wasiliana nasi Makazi Fumigation & Hygiene Services kupitia:

📞 0685 482 846