Namna ya Kudhibiti Mijusi Nyumbani
Mijusi huvutiwa zaidi na wadudu kama mbu, nzi na viroboto. Ukipunguza wadudu, unapunguza pia mijusi. Pia wana tabia ya kujificha kwenye maeneo yenye giza na joto. Hapa ni hatua za uhakika:
1. Punguza Vyanzo vya Chakula (Wadudu)
- Fanya usafi wa mara kwa mara ili kupunguza wadudu wanaovutia mijusi.
- Fanya fumigation ya ndani na nje ya nyumba ili kuua mbu, nzi, mende na wadudu wengine wanaowavutia mijusi.
- Usiachie chakula wazi ndani ya nyumba.
2. Zuia Njia Wanazotumia Kuingia
- Funga madirisha vizuri au tumia neti za madirisha zenye mesh ndogo.
- Ziba nyufa kwenye kuta, nyuma ya makabati, chini ya milango na pembe za paa.
- Hakikisha paa halina mianya inayowawezesha kuingia.
3. Ondoa Mazingira Yenye Mazalia
- Ondoa makaratasi yasiyotumika, maboksi, magodoro ya zamani, na vitu vilivyoharibika vinavyoweza kuwa maficho.
- Safisha nyuma ya friji, makochi na kabati — mijusi hupenda joto na giza.
4. Tumia Mbinu za Asili
- Ganda la mayai: Weka vipande vya ganda la yai kwenye kona za nyumba. Harufu yake huwafanya mijusi waondoke wakidhani kuna adui.
- Pilipili manga au pilipili kali: Changanya maji na pilipili kali, kisha nyunyiza kwenye maeneo yao. Harufu huwafukuza.
- Vitambaa vya harufu kali (camphor): Vifunika kidogo kwenye kona; harufu yake haipendwi na mijusi. (Usiweke sehemu watoto wanaweza kufikia.)
5. Tumia Vizuia Mijusi (Repellents)
Kuna dawa maalum zinazotumika kuzuia mijusi kupita au kukaa kwenye maeneo fulani.
- Zinaweza kupakwa ukutani au kunyunyizwa.
- Inafanya kazi kuzuia, sio kuua, lakini hupunguza uwepo wao kwa kiasi kikubwa.
6. Fumigation ya Kitaalamu
Kwa nyumba zenye kero kubwa:
- Fanya fumigation ya kitaalamu ndani na nje ya nyumba.
- Fumigation huondoa chanzo chao kikuu — wadudu.
- Hii inapunguza uwepo wa mijusi kwa kiwango kikubwa na cha kudumu.
7. Usafi wa Mara kwa Mara
- Safisha mabakuli ya mbwa/kuku baada ya kula, kwani mabaki ya chakula huwavutia wadudu na baadaye mijusi.
- Osha maeneo yenye unyevunyevu kama jikoni, sinki na bafu.
Kwa Huduma na Ushauri Zaidi
Ikiwa mijusi imekuwa kero kubwa, unaweza kupiga simu Makazi Fumigation & Hygiene Services kwa matibabu ya kitaalamu na ushauri sahihi.
📞 0685 482 846
